Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanroads yasema haijabadili mchoro ujenzi wa flyover Ubungo

14444 Mchoro+pic TanzaniaWeb

Wed, 29 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale amesema hawajabadili mchoro wa ujenzi wa barabara ya juu (Interchange) eneo la Ubungo, walichokifanya ni kuboresha.

Mfugale ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti 29, 2018 wakati akijibu swali la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyetaka kujua kama mchoro umebadilishwa au la.

“Hatukubadili mchoro bali tumeuboresha na huu ndio sahihi na mzuri kuliko ule wa awali,” amesema Mfugale wakati akimjibu Majaliwa ambaye leo amefanya ziara kukagua ujenzi huo.

Katika ufafanuzi wake Mfugale amesema hadi kufikia Juni, 2020 barabara hiyo itakuwa imekamilika na itakuwa na ngazi tatu.

Kuhusu changamoto ya uwepo wa wafanyabiashara katika eneo la Ubungo unapofanyika ujenzi huo, Majaliwa amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusimamia zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz