Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani milioni 10 za tumbaku kununuliwa Chunya

TUMBAKU Tani milioni 10 za tumbaku kununuliwa Chunya

Wed, 20 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kilio cha ukosefu wa soko la tumbaku kwa wakulima Wilaya ya Chunya Mkoa Mbeya kimepata ufumbuzi baada ya Kampuni ya Mkwawa Leaf, kuingia mkataba wa kununua tani 10 milioni kwa mwaka.

Akizungumza leo Jumatano Julai 20, 2022 Mbunge wa Lupa, Masache Kasaka baada ya kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mkwawa Leaf, Richard Sinamtwa ya kuanza ununuzi wa zao hilo.

Pia ameahidi kusaidia upatikanaji wa pembejeo za kilimo, mabanio sambamba na wataalam wa kilimo   ili kuwawezesha kuzalisha kwa tija na kukausha kwa ubora.

“Kwa sasa kampuni zimeanza kuingia kwa wakulima na zao hilo ambalo litauzwa kupitia vyama vya ushirika lengo kuu ni kuona mkulima ananufaika na kuacha kunyonywa na wachuuzi ambao walikuwa ni changamoto kubwa kilio kwa muda mrefu,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mkwawa Leaf, Richard Sinamtwa matarajio yao ni kuona uzalishaji kwa wakulima unaongezeka na uwepo wa tumbaku ya kutosha ili kuwezesha mtambo wa kusindika tumbaku kutosimama uzalishaji mara baada ya kuzinduliwa.

Amesema lengo ni kukusanya tumbaku kwa wingi huku ikiwa imeingia ubia na vyama vya msingi vya wakulima vinne kupitia Chama cha Wakulima wa Tumbaku Chunya (Chutcu).

Advertisement Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera akiitambulisha rasmi Kampuni hiyo kwa niaba ya Wizara ya Kilimo, alihamasisha vyama vya msingi vya wakulima kujisajiri ili kuweza kuuza tumbaku kwa makampuni yanayoingia kwa ushindani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live