Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 98,800 za korosho zauzwa Mtwara, mapato yafika Tsh.bil 222

KOROSHO 2 Tani 98,800 za korosho zauzwa Mtwara

Thu, 2 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakulima mkoani Mtwara wameuza zaidi ya tani 98,800 za korosho kwa Sh bilioni 222 tangu msimu wa mauzo kupitia minada iliyoanza mapema mwezi Oktoba.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brig. Jen. Marco Gaguti amewaambia waandishi wa habari kuwa mkoa huo unategemea kuuza zaidi ya kiasi kilichouzwa mwaka jana cha tani 118,000.

“Tumejipanga kuhakikisha wakulima wanaongeza tija kwenye zao la korosho. Wataalamu wamebainisha kuwa ukiongeza thamani unapata fedha mara nne zaidi ya bei ambayo ungeuza bila kuongeza thamani,” alisema Brig. Jen. Gaguti.

Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa mkoa umejipanga kufundisha vikundi vya wakulima na wajasiliamali kwa msimu wa kilimo ujao ili waweze kuongeza thamani katika zao la korosho.

Katika hatua nyingine, Brigedia Jenerali Gaguti amewata wakulima wa zao la korosho na wananchi wa mkoa huo kuhakikisha wanawekeza kwenye swala la akiba ya chakula.

Pia amewaomba kufikiria kulima mazao ya muda mfupi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya uhaba wa chakula, huku akibainisha kuwa Mkoa wa Mtwara umepanga kuweka mkakati ambao utawawezesha wafanyabiashara wadogo wakiwemo bodaboda, kuweza kuinua mapato yao zaidi.

Amesema wafanyabiashara hao watapewa elimu kuhusu masuala ya fedha na uwekezaji na kufundishwa jinsi ya kuanzisha miradi mikubwa ya biashara, ambayo itawasaidia kujiongezea kipato chao.

Amesema pia wafanyabiashara hao hasa bodaboda kupitia elimu ya fedha, watawezeshwa kuanzisha mifuko ya fedha ambayo itawasaidia kupata mikopo wao wenyewe na kuanzisha miradi ya maendeleo mbali na kujishughulisha na biashara za kubeba abiria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live