Jumla ya tani 89,658 za korosho ghafi zenye thamani ya Sh bilioni 169.82 zimeuzwa katika minada iliyoanza Octoba 28 mwaka huu.
Kaimu Mkurungezi wa Masoko na Udhibiti Ubora wa Bodi ya Korosho Nchini (CBT) Domina Mkangara amesema korosho hizo ziliuzwa katika minada 20 kati ya 26 iliyofanyika tangu kuanza kwa msimu wa mauzo.
"Tulianza minada Octoba 28 ambapo minada sita ya awali wakulima hawakuridhia kuuza korosho zao na mpaka sasa tumefanya jumla ya minada 26," amesema Mkangara.
Mkangara amesema wakulima walikataa kuuza korosho zao kutokana na bei kuwa chini. Katika minada ya awali bei ya korosho kwa kilo ilikuwa kati ya shilingi 1650 na shilingi 2200.