Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 67,393 za vioo zauzwa nje ya nchi

Kijajipic Data Tani 67,393 za vioo zauzwa nje ya nchi

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa kiwanda cha Kioo Limited kwa mwaka 2023 kilizalisha bidhaa za chupa zenye uzito wa tani 131,105 nakuuza nje ya nchi yetu tani 67,393 za viookatika nchi mbalimbali zikiwemo DRC, Malawi, Zimbabwe, Uganda, Rwanda, Kenya nanchi za Bara laUlaya.

Dkt. Ashatu ameyasema hayo Leo mei 21, 2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hoja ya Bajeti ya Makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2024/2025 ya Wizara ya Viwanda na Biashara

Aidha, Dkt. Ashatu amesema kuwa kiwanda hicho kimewekeza kiasi cha shilingi bilioni 4.4 nakutoa ajira za moja kwa moja 613.

Dkt. Ashatu amesema kuwa asilimia 80 ya malighafizinazotumika na kiwanda hicho zinatoka ndani ya Tanzania.

Dkt. Ashatu ameongeza Kwa kusema kuwa Taifa la Tanzania lina nafasi kubwa ya kunufaika na masoko ya kikanda kama EAC, SADC na AfCFTA ambayotumeanza kunufaika kwa kiwango kikubwa na masoko haya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live