Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 664 bidhaa zisizo na ubora zateketezwa tangu 2015 nchini Tanzania

87262 Dawapic Tani 664 bidhaa zisizo na ubora zateketezwa tangu 2015 nchini Tanzania

Thu, 5 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tani 664.6 za bidhaa za dawa na vifaa tiba zimeteketezwa mwaka 2018/19 kutokana na kutokidhi viwango vya ubora.

Kiwango hicho kimeelezwa kupungua ikilinganishwa na tani 140,705.2 za mwaka 2017/2018.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Desemba 5, 2019 na kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo wakati akieleza mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne.

Amesema kupungua kwa bidhaa hizo zilizoteketezwa inaashiria kufanikiwa katika mapambano ya bidhaa zisizokuwa na ubora kuingia sokoni.

Amesema katika kutekeleza hilo, sampuli 1136 ya dawa za binadamu zilifuatiliwa na kuchunguzwa katika kipindi hicho cha miaka minne na kwamba asilimia 96 kati ya zilizochunguzwa zilikidhi viwango vya ubora.

“Kati ya sampuli zote zilizofuatiliwa na kuchunguzwa ni asilimia 4 pekee ndio zilionekana hazikidhi viwango vya ubora na ziliondolewa sokoni. Hii inaashiria kuzidi kupungua kwa bidhaa zisizokidhi viwango katika soko la Tanzania,” amesema.

Pia alizungumzia kuhusu mifumo ya udhibiti na ufuatiliaji wa madhara yatokanayo na matumizi ya dawa na vifaa tiba ili kuweza kuchukua hatua.

Amesema katika hilo wameanzisha mfumo wa kielektroniki wa upokeaji wa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwa kutumia simu za mkononi au  kompyuta.

Chanzo: mwananchi.co.tz