Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 500 za mahindi kusambazwa

GUNIA.jpeg Wakala wa mbegu bora za kilimo nchini ASA imesema kwamba msimu wa kilimo 2021/2022 imekusudia kusamb

Sun, 3 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

Kauli hiyo ilitolewa jana na meneja wa shamba la mbegu bora za kilimo la Kilimi wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Jacob Chiwanga wakati akipokea tani 80 za mbegu katika kituo cha reli mkoani Tabora jana.

Alisema kwamba kutokana na mahitaji ya wakulima kanda hiyo imewalazimu kuanza kusambaza mbegu hizo mapema kwa ajili ya wakulima kuwahi mandalizi ya msimu wa kilimo.

Chiwanga aliendelea kusema kwamba Asa kwa kanda hizi mbili itasambaza mbegu hizo kwa njia ya  reli ili kupunguza gharama za usafiri  ,kwani usafiri wa reli ni rahisi sana tofauti na kukodi magari .

“Tani hizo 80 kama wangetumia usafiri wa malori yangetumika  zaidi ya magari 8 ya tani kumi   jambo ambalo Gharama zingeogezeka mara dufu”alisema Chiwanga

Hata hivyo alisema kwamba kwa upande wa wilaya na mikoa ambayo ipo kando ya barabara kuu ya kanda  wataendelea kusafirisha kwa magari ambapo hada sasa wamesha sambaza tani 30 katika wilaya za Igunga ,Nzega na upande wa mikoa ya ziwa.

 Mfanyabiasha wa Pembejeo wilaya ya Nzega Mkoani Tabora John Songo  alisema kwamba ASA   ni mara ya kwanza kusambaza mbegu kwa njia ya Reli  jambo ambalo linaonesha wakala amedhamiri kuwasaidia wakulima wa mazao mbalimbali yanayosazalishwa na ASA.

Alisema hali hiyo itasaidia kupunguza bei za mbegu bora za kilimo zinazosambazwa na ASA katika mkoa wa Tabora.

Naye mfanyabiashara Yuda Mayila alipongeza  wakala kwa kuanza kusafirisha pembejeo  kwa njia ya Reli kitu ambacho kitasaidia sana kupunguza  Gharama za kuwafikia walaji ambao ni wateja.

Hata hivyo Hakidum Mkuyu ambaye ni miliki wa duka la Pembejeo la Kachoma la mjini hapa alisema hilo ni jambo la kheri kwani walikuma mwaka huu watanufaika sana kwa bei ndogo za mbegu bora za mahaindi hasa Situka M .1  zinazosambazwa na wakala wa mbegu bora za kilimo nchini ASA.

Chanzo: ippmedia.com