Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 500,000 za mihogo kupitishwa bandari ya Tanga

Tanga Bandaric4 88ce 563406428007 780x470 Tani 500,000 za mihogo kupitishwa bandari ya Tanga

Wed, 9 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni kubwa ya Afritech Greencrops Group ya nchini China inatarajia kupitisha tani laki tatu za Mihogo kutoka wilaya ya Handeni kupitia bandari ya Tanga kwenda nchini China.

Akizungumza katika wa kilele cha maonyesho ya Wakulima Nanenane Kanda ya Mashariki mkoani Morogoro alipotembelea banda la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Meneja Msaidizi wa Kiwanda hicho William Zhang amesema ndani ya miezi tisa kutoka sasa waatanza kusafirisha bidhaa hizo.

Zhang amesema kuwa watapitisha bidhaa hiyo katika bandari kwa sababu imefanyiwa maboresho makubwa sana ikiwemo kuwa na vifaa vipya vya kupakulia mizigo bandarini.

Katika ziara hiyo Meneja huyo alifuatana na Wakulima wa mihogo pamoja na Madiwani wa halmashauri ya wilaya Handeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live