Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 4,000 za sukari zatua bandarini

Sukarii Sukari Leseni Tani 4,000 za sukari zatua bandarini

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MELI mbili zilizobeba shehena ya sukari zaidi ya tani 4,000 zimeingia nchini na tayari meli moja imeanza kupakua bidhaa hiyo.

Kadhalika Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) imesisitiza kuwa bei elekezi ya sukari ni kati ya Sh 2,700 hadi 3,200 na kuwa bei hiyo ni sheria hivyo wafanyabiashara wote wasiofuata sheria hiyo wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza , Mkurugenzi Mkuu wa SBT, Profesa Kenneth Bengesi alisema meli hizo mbili ziliingia nchini juzi na moja imeanza kushusha sukari ambayo inaenda moja kwa moja sokoni.

“Kuna meli mbili zimeingia leo (juzi) na shehena ya sukari karibu tani 4,000, zinapofika tu nchini, bandari inatupa kipaumbele, meli zinaingia kushusha kwa sababu ya uhitaji wake katika jamii, hivyo hazikai kusubiri,” alisema. Profesa Bengesi alisema awali Januari 29, mwaka huu, meli nyingine iliingia nchini ikiwa na shehena ya sukari na ilikamilisha utaratibu wa kiforodha na kuanza kushusha sukari Januari 30 na 31.

“Hivyo kwa meli zote, ile ya kwanza ukijumuisha na hizi mbili ina maana karibu tani za sukari 5,000 zimeingia nchini,” alisema. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live