Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 29 za tende zateketezwa Zanzibar

Tende Znz Shehena ya Tende ikiteketezwa

Mon, 7 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya chakula dawa na vipodozi ZFDA imesema jumla ya tani 29 za tende ya kula iliyomalizika muda wake imeteketezwa huko katika jaa la Kibele Unguja.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uteketezaji wa bidha hiyo Mkaguzi Mkuu wa Chakula na utekelezaji Suleiman Akida Ramadhani amesema tende hizo zilizomaliza muda wake zimegundulika huko katika ghala bubu ilioko Kilimahewa na kujulikana na wasamaria wema.

Pia amesema wananchi waligundua kwa kusikia harufu na nyengine kutupwa mitaani katika sehemu za Welezo na haraka kupeleka taarifa kunakohusika na kuchukuliwa hatua za haraka.

Amesema iko haja ya kutolewa elimu kwa wafanyabiashara wanaoleta bidhaa zilizokuwa zimeshamaliza muda wake kuacha tabia hiyo kwani inaweza kuathiri jamii kwa kutumia bidhaa hizo.

Aidha amesema bidhaa hiyo itakapotumika itaweza kuathiri afya ya mlaji kwa kemletea madhara makubwa athari hizo ni pamoja kupata madhara ndani ya mwili .

Pia amesema mfanyabiashara aliyehusika na bidhaa hiyo ni Hafidh Salim Ali na kulipia gharama zote za utekelezaji huo.

Nae Afisa Mazingira kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Mambo ya hali ya hewa Lailati Mussa Foum amesema bidhaa zilizoharibika zinahitaji kuteketezwa kwa haraka kwani sio sahihi kutumika kwa jamii.

Hivyo amesema wafanyabiashara wahakikishe wanaoleta bidhaa zilizokuwa salama kwa matumizi, ziwe na viwango na iwapo zitagundulika kubakia muda mdogo kumalizika zisiingizwe nchini kwani hazitoruhusiwa .

Kwa upande wa wananchi wameishukuru Bodi ya chakula ,dawa na vipodozi kwa kuchukua hatua za haraka kuteketezwa bidhaa hiyo hasa ukizingatia mwezi mtukufu wa Ramadhani unakaribia na kuogopa isije ikatumika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live