Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 250,000 za Korosho kusafirishwa kwa Bandari msimu wa 2021/2022

Mtwara Korosho Kuelekea msimu wa Korosho wa mwaka 2021/2022

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imeongeza muda wa kuhifadhi makontena bandarini kutoka siku saba kwa makontena tupu hadi siku 21 na siku saba kwa makontena yenye mizigo hadi siku 14 kwa mikoa yatakayotumia bandari ya Mtwara.

Uamuzi huo umefikiwa kufuatia agizo la Rais, Samia Suluhu Hassan kuitaka TPA kutumia bandari ya Mtwara kusafirisha korosho zinazozalishwa kwenye mikoa hiyo mitatu.

Meneja wa bandari ya Mtwara Mhandisi Juma Kijavara amesema bandari hiyo inatarajia kusafirisha tani zaidi ya 250,000 za korosho kutoka katika mikoa hiyo kati ya tani 280,000 zinazotarajiwa kuzalishwa katika mikoa hiyo kwa msimu wa mwaka 2021/2022.

Katibu Tawala wa wilaya ya Mtwara, Thomasi Salala amewataka wananchi kuthamini zao la korosho kwani zao hilo linaingiza fedha za kigeni nchini.

Biashara ya Korosho kwa sasa ni nzuri huku Bei ya korosho ghafi katika soko la minada chini ya mfumo wa stakabadhi ghalani ukiendelea kuimarishwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live