Zaidi ya tani 20,000 za Korosho ghafi zinatarajiwa kupigwa mnada katika sehemu mbalimbali zinazolima zao hilo ikiwa ni msimu wa mauzo kwa mwaka 2022/23, Kaimu Mkurungezi wa wa Bodi ya Korosho Nchini (CBT) Alfred Francis amesema mkoani Mtwara.
Minada ya korosho hizo itaanza leo na kumalizika Nov. 3, 2022. Mnada utakaofunguliwa leo ni wa pili na utahusisha zaidi ya tani 15,000 ya korosho ambazo hazikuuzwa wakati wa mnada wa kwanza ulioahirishwa kwa sababu za bei ndogo iliyotangazwa na wanunuzi.
Mbunge wa Masasi mkoani Mtwara Cecil Mwambe alishauri serikali kuondoa baadhi tozo kwenye zao la Korosho ili kumwezesha mkulima kuuza na kupata faida katika Minada ambayo inaendelea nchini.
Wakulima wa korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara walikataa kuuza korosho katika mnada wa Oktoba 22 wakidai kiasi kilichotangazwa hakiendani na gharama za uzalishaji.
Vyama vikuu vya ushirika vya TANECU, MAMCU, RUNALI na Lindi Mwambao, vilitangaza bei ya juu ya korosho kwa kilo ikiwa Sh 2,200 na bei ya chini Sh 1,480.