Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 16,000 mahindi zadaiwa kukosa soko

Maize   Monyo Tani 16,000 mahindi zadaiwa kukosa soko

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

TANI 16,000 za mahindi wilayani Ludewa mkoani Njombe, zinadaiwa kukosa soko endapo ununuzi wa mahindi na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) utafungwa baada ya kununua tani 1,000 pekee.

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Joseph Kamonga, baada ya kutembelea kituo cha ununuzi wa mahindi kilichoko kijiji cha Mlangali na kupokea kero mbalimbali kutoka kwa wakulima waliofika na kuuza mazao yao.

“Ukiacha chakula, tuna tani za ziada 17,000 za mahindi, lakini NFRA wamenunua tani 1,000 pekee kwa hiyo tani 16,000 zinakosa soko,” alisema Kamonga.

Alisema nia kubwa ya kutembelea kituo hicho ni kutokana na malalamiko mengi aliyokuwa akiyapokea kutoka kwa wananchi wakati akiwa jijini Dodoma.

“Nia yangu ya kuja hapa ni kutokana na malalamiko mengi ambayo nikiwa bungeni Dodoma nilikuwa nikiyapokea kila siku mpaka hapakaliki. Kwenye bei pia mahindi yananunuliwa shilingi 430 kwa kilo, mwanzoni wananchi walishangilia waliposikia yanauzwa 500 kwa kilo, lakini baadaye yakaanza mabadiliko ya bei hii imeleta malalamiko sana kwa wakulima na wanahofu hapa katikati imebadilisha kumbe toka mwanzo wangekuwa wametoa bei elekezi kwa kila eneo hii ingepunguza malalamiko,” alisema Kamonga.

Alisema wananchi wakulima wamekuwa na kero ya kusafiri umbali mrefu wengine kilomita 78 kufuata kituo cha ununuzi wa mahindi kilichopo kijiji cha Mlangali huku awali katika wilaya hiyo kulikuwa na vituo vitatu.

“Kwa miaka mingi Ludewa kumekuwa na vituo vitatu, kituo cha Ludewa vijijini, Mlangali pamoja na kituo cha Shaurimoyo na hii imekuwa ikiwarahisishia wakulima kufikisha mazao kwenye soko kirahisi, lakini kwa sasa tumewaongezea mzigo mkubwa sana wakulima,” aliongeza Kamonga.

Alisema wananchi wana imani kubwa na ununuzi wa mahindi unaofanywa na NFRA huku akiahidi kushughulikia kero zilizojitokeza ili kuwasaidia wakulima wa Jimbo la Ludewa.

Chanzo: ippmedia.com