Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 130 za korosho zimenunuliwa

28440 Tani+pic TanzaniaWeb

Fri, 23 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mtwara. Mpaka sasa, Serikali imeshanunua jumla ya tani 130.11 za korosho zilizokusanywa kutoka halmashauri mbalimbali za mikoa ya Lindi, Ruvuma na Mtwara na takriban Sh5 bilioni zimeshatumika kuwalipa wakulima.

Akitoa tathmini ya ununuzi wa zao hilo ambao msimu huu unafanywa na Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelisius Byanakwa alisema tayari vyama 83 vimefanyiwa uhakiki ili malipo yote yawanufaishe wakulima kama ilivyoelekezwa.

Baada ya wanunuzi kugoma kununua korosho kwa Sh3,000 kwa kilo wakisema soko lake limeporomoka msimu huu, Serikali iliamua kununua yenyewe kwa Sh3,300 kwa kilo huku ikihamasisha ujenzi wa viwanda vya ubanguaji ili kuondokana na usafirishaji wa korosho ghafi.

“Malengo ya kukusanya na kununua korosho kwa msimu huu yatafanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuwa wadau mbalimbali hususan viongozi wa vyama vya msingi wameonyesha ushirikiano wa kutosha,” alisema.

Inakadiriwa kuwa mavuno ya korosho msimu huu yatakuwa tani 210,000 na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imepewa jukumu la kununua zao kwa usimamizi wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likiwa na dhamana ya kusafirisha bidhaa hiyo kutoka huko na kuzipeleka Dar es Salaam.

Ahadi ya Magufuli

Novemba 12, Rais John Magufuli alisema Serikali itanunua korosho zote za wakulima zilizolimwa msimu huu na kuzitafutia soko.

Alitangaza uamuzi huo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha mawaziri na manaibu waziri ambao aliwateua Novemba 10.

Aliipa JWTZ jukumu la kuhakikisha mchakato wa nununuzi na usafirishaji wa korosho unafanyika kwa mafanikio makubwa.



Chanzo: mwananchi.co.tz