Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tangazeni mafanikio ya uwekezaji

Uchumi Kupanda Tangazeni mafanikio ya uwekezaji

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Mazingira ya Biashara kutoka wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Baraka Aligaesha amewashauri Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kutangaza na kuuelimisha umma kuhusu utekelezaji wa mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini (MKUMBI).

Baraka ametoa ushauri huo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa mpango huo na mafanikio yake katika kikao kazi cha 18 cha Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) kinachoendela mkoani Dar es Salaam.

Amesema, ni jukumu la kila Afisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kutangaza na kuelimisha umma kuhusu maboresho yanayotokea katika sekta husika kutokana na utekelezaji wa MKUMBI, ili kuvutia wawekezaji na kuhamasisha ufanyaji biashara nchini.

Chanzo: mwanachidigital