Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanga kuzalisha katani tani 60,000

Cea496bfe78c20102fb002969da08bfa Serikali imeshaandaa vituo 753 kwaajili ya waliopata ujauzito wakiwa shule

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima, amesema mkoa huo umejipanga kufufua zao la mkonge kwa kasi huku akiweka matarajio ya kuzalisha tani 60,000 za katani inayotokana na zao hilo kwa mwaka.

Amesema miaka 50-55 iliyopita, Tanga ilikuwa inazalisha zaidi ya tani 1,500,000 za katani ambapo kwa sasa imeshuka hadi kufikia tani 20,000.

Malima amesema hayo jijini Tanga leo wakati akizungumza na Wanachama na Wadau wa Chama cha Mkonge Tanzania (SAT).

"Lengo la Mkoa wa Tanga ni kufikia tani 60,000 ndivyo tulivyojiwekea mimi, halmashauri na wadau wangu kwa ujumla.” amesema na kufafanua

“Yaani kabla hatujaenda kwenye uchaguzi mkuu ujao tunataka Mama Samia (Rais Samia Suluhu) asimame kama Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) awaambie watu wa Tanga kwamba kwenye tani hizo 100,000 ambazo zimelimwa kitaifa, tani 60,000 zimetoka kwenye Mkoa wa Tanga kwa sababu tani 60,000 ni kama Sh bilioni 2 ambazo ukiongeza kwenye kipato cha mkoa ni fedha nyingi sana.

"Kwa hiyo hayo ndiyo matarajio yetu kwa sababu unajua kuna kutaka na kufanya, tunaweza tukataka kwamba tunataka tufikishe tani 60,000 ifikapo miaka mitano ijayo lakini uipangie mikakati kwa hiyo mikakati tumejipangia na nafasi ya kila mmoja kama serikali kuu, serikali ya mkoa, halmashauri na wadau kwa maana ya Wizara ya Kilimo katika kufikia malengo hayo," amesisitiza

Aidha, Malima amesema katika malengo hayo wamegawana majukumu kwenye uzalishaji huo ambapo wakulima wadogo na wa kati Mkoa wa Tanga wanatakiwa kuzalisha tani 10,000-15,00 na wakubwa wazalishe tani 30,000-40,000.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge, Saad Kambona amesema katika katika mazungumzo hayo wamekubaliana kutekeleza malengo ya serikali kuongeza uzalishaji kufikia tani 120,000.

Chanzo: www.habarileo.co.tz