Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanga cement yapoteza shilingi bilioni 7.8 kwa miezi 6

Tngcmntddd Tanga cement yapoteza shilingi bilioni 7.8 kwa miezi 6

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya uzalishaji saruji ya Tanga 'Tanga Cement' imepoteza zaidi ya asilimia 50 ya mapato katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa mwaka 2021, kufuatia kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Jumla ya shilingi bilioni 2.6 zimeongezeka katika upotevu huo tofauti na kiasi kilichopotea kwa mwaka 2020 na kupelekea kufika asilimia hizo 50 za upotevu kwa mwaka 2021.

Kufuatia majibu ya wakaguzi wa mapato na matumizi waliofanya ukaguzi kwa miezi sita ya mwanzo imeonesha kuwa kampuni hiyo imepoteza shilingi bilioni 7.8 ndani ya miezi hiyo kwa mwaka 2021 kutoka kupoteza shilingi bilioni 5.2 mwaka 2020.

Nae Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo, Lawrence Masha, amesema kuwa changamoto za kifedha ndizo zimesababisha kushuka kwa uzalishaji jambo amablo limepelekea kupoteza kiasi hicho kikubwa cha pesa.

Mapato ya kampuni hiyo kwa kipindi cha miezi sita ya awali ni shilingi bilioni 89.21 kutoka shilingi bilioni 94.32 kwa mwaka 2020.

Kufuatia hali hii bodi ya wakurugenzi imefikia maamuzi ya kutogawana faida ya hisa walizowekeza badala yake fedha hizo zitakusanywa ili kutumika kuongeza uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live