Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanga: BRELA watoa elimu maonesho ya Biashara, Utalii

IMG 20240602 WA0014 Tanga: BRELA watoa elimu maonesho ya Biashara, Utalii

Sun, 2 Jun 2024 Chanzo: dar24

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni – BRELA, wameendelea na zoezi la kutoa Elimu kwa Wafanyabiashara na Wananchi pamoja na kufanya huduma mbalimbali za kusajiri Makampuni, kusajiri majina ya alama za Biashara, kusajili Leseni za Biashara.

Afisa Usajili kutoka BRELA, Julieth Kiwelu amewaeleza Waandishi wa Habari mapema leo kuwa, huduma zote ambazo hutolewa ofisini kwao kwasasa zinatolewa kwenye maonyesho hayo ikiwemo kutoa Leseni za viwanda pamoja na hataza, katika maonesho ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga.

Amesema, “huduma zote zinazotolewa ofisini kwetu kwasasa zinapatikana kwenye maonyesho haya ya Biashara na Utalii,hivyo tunawaomba Wafanyabiashara na Wadau mbalimbali waje hapa wapate huduma zote ambazo hutolewa ofisini kwetu.

Ofisa Usajiri kutoka Wakala wa Usajili na Biashara Nchini – BRELA, Julieth Kiwelu (kulia) akimkabidhi cheti cha Usajili wa Biashara mfanyabiashara, Ismail Mashauri kutoka kijiji cha Mtimbwani wilayani Mkinga, wakati wa maonyesho ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga.

“Kazi kubwa ya maonesho haya ni kutoa Elimu na huduma kwaufumbuzi na alama za Biashara na huduma,kwetu sisi tumeichukulia hii kama fursa ya kutoa Elimu na tukumbuke kuwa sehemu ya Elimu hii ni uvumbuzi na sisi BRELA,” amesema Julieth.

Ameongeza kuwa, “uvumbuzi ndio kazi kubwa tunayoifanya ,wengi hawafahamu nini cha kufanya baada ya kuvumbua kitu , kwahiyo tunachokifanya nikuwapatia Elimu sahihi  wa Biashara na Leseni nakuwataka wadau mbalimbali kuhakikisha wanasajili huduma mbalimbali wanazozitoa.”

“Tunawaomba wadau wetu wasajiri huduma wanazozitoa ili ziwe na vibali ,na sisi tupo tayari wakati wowote kutoa huduma,na tutaendelea kushirikiana na Wadau wetu na wasichoke kutuuliza pale wanaposhindwa kutimiza vigezo” alifafanua Julieth.

Amesema kwasasa kusajili Biashara na kupata Leseni za ‘BRELA’ ni rahisi na wanaweza kupata huduma kwanjia ya mtandao, kwani unaweza kupata huduma kwa njia ya mtandao, huku wakiwaomba wavumbuzi kuacha kusikiliza maneno ya mtaani yanayowapotosha na watapata Elimu isiyo sahihi.

Chanzo: dar24