Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanesco wapewa maagizo mapya

UMEME Vunjwa Tanesco wapewa maagizo mapya

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kuboresha mfumo wa utoaji huduma kwa wateja ili kupunguza malalamiko na kuwapatia wananchi hao huduma ya umeme kwa wakati.

Kapinga ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya uzalishaji wa umeme katika Kituo cha Kuzalisha Umeme Megawati 43 kwa kutumia Gesi Asilia cha Tegeta, Jijini Dar Es Salaam tarehe 2 Octoba, 2023.

Akizungumzia kituo hicho Kapinga amesema hali ya uzalishaji ni nzuri na kwamba kituo hicho kina mitambo mitano, mmoja kati ya hiyo uko kwenye matengenezo.

Amesema mfumo bora wa utoaji huduma kwa wateja hutatua changamoto ndogondogo zinazowakabili wateja majumbani kwao kama vile kuungua ama kuharibika kwa waya, Umeme kukatika, matatizo ya LUKU pamoja na kuharibika kwa Mashine.

“Haipendezi na hatutakubali mwananchi yeyote alale giza kwa sababu tu hajahudumiwa licha kuwa ametoa taarifa kutokana na changamoto inayomkabili, ama changamoto yake haijatatuliwa kwa wakati, na wakati mwingine hapati majibu sahihi juu ya changamoto yake, hivyo TANESCO imarisheni mifumo yenu ili wananchi wapate huduma kwa wakati”, Amesisitiza Kapinga.

Vilevile ameliagiza Shirika hilo kuwaunganishia umeme wananchi wote waliopo katika maeneo ambao tayari yamefikiwa na miundombinu ya umeme na uunganishwaji huo ufanyike kwa haraka na kwa wakati ili wananchi wafurahie huduma ya upatikanaji wa Umeme.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live