Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanesco kuanza kutumia huduma ya ni-conekt

Tanescopiic Data Tanesco kuanza kutumia huduma ya ni-conekt

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mkoa wa Simiyu limeanza kutumia mfumo wa kielectroniki wa ni-konekt ili kurahisisha huduma kwa wateja wapya pamoja na kupunguza msongamano wa gharama na muda pindi wanapohitaji huduma za kuunganishiwa umeme.

Akizungumza na mafundi umeme wanaotandaza mfumo wa umeme majumbani Meneja wa tanesco Mkoa huo, Alistidia Clemence amesema mfumo huo utaanza kutumia Juni 6, 2022 ambapo wateja watatuma maombi popote walipo.

"Faida za mfumo huu ni kurahisisha na kuondoa vishoka ambao walikuwa mtu kati katika utoaji wa huduma kwa wateja na itaondoa usumbufu na gharama za mteja kuja na kurudi katika ofisi zetu ili kukamilisha huduma za usafiri" amesema

Mhandisi Johansen Mukulasi akimwakilisha mhandisi mkuu wa ufundi amesema wanachokisisitiza kwa mafundi hao ni ufanisi na kuhakikisha wanakizi vigezo vya usajili ili kutoa huduma bora kwa wateja.

Hapo awali mfumo uliotumika ulitaka mteja kutembelea ofisi za Tanesco Ili apate fomu ya maombi pamoja na kufuatilia usajili ambao ulichukua siku 30 Hadi 90 ili mteja kupata huduma ya umeme.

"Ilikuwa mteja Ili apate umeme ni lazima afike ofisi za Tanesco na muda mwingine arudi bila kuhudumiwa kwa sababu ya changamoto za mtandao na pengine akimaliza itachukua muda mrefu hadi kuwashiwa umeme hali iliyosababisha sisi mafundi tuonekane matapeli" amesema Joseph Ikombe fundi umeme.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live