Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanapa tumieni teknolojia kulinda hifadhi

Waziri Kairuki Awataka Walimu Nchini Kufuata Taratibu Za Waraka Namba 24.jpeg Tanapa tumieni teknolojia kulinda hifadhi

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ameliagiza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kutumia teknolojia ya kisasa kulinda na kuhifadhi maeneo yake kwa lengo la kuzuia ujangili na uvamizi wa maeneo hayo.

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo akizungumza na menejimenti ya TANAPA kwa lengo la kupanga namna ya kulinda hifadhi za Taifa.

"Kuhusu kukabiliana na ujangili pamoja na kufanya doria hifadhini tuendelee kuwa na matumizi ya vifaa vya teknolojia ya kisasa kuhakikisha doria na ulinzi wa maeneo yetu unafanikiwa kwa asilimia 100,"amesema.

Ameeleza kuwa kufanya hivyo itawarahisishia utendaji kazi na kuwezesha ulinzi wa maeneo ya hifadhi kwa njia ya kisasa zaidi.

Kaimu Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Mussa Juma ameahidi kuendelea na Uwekezaji katika ulinzi wa hifadhi na kuzitangaza zaidi kwa lengo la kuongeza idadi ya watalii wanaozitembelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live