Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TanTrade yapokea vifaa vya Sabasaba

Sabasaba Sabasaba (600 X 380) TanTrade yapokea vifaa vya Sabasaba

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Latifa Khamis amepokea udhamini wa viti, meza na vizimba 170 vya mabanda ya maonesho, vyenye thamani ya shilingi Milioni 300 kutoka kampuni ya East Africa Commercial and Logistic Center (EACLC), ambayo pia ni wadhamini wakuu wa maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu Sabasaba.

Akizungumza katika makabidhiano ya vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Latifa Khamis amesema, Mamlaka hiyo imeokoa zaidi ya shilingi Milioni 100 zilizokuwa zinatumika kukodisha vifaa hivyo ili kukidhi mahitaji ya washiriki katika maonesho hayo.

Kwa upande wake meneja Mkuu wa kampuni ya EACLC Wang Xiangyu amesema, wamefarijika kuwa wadhamini Wakuu wa maonesho hayo kwa mwaka huu na hiyo ni hatua ya mwanzo ya ushirikiano kati ya TanTrade na kampuni hiyo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live