Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taliri yaanzisha vituo 30 ufugaji

5832f78dd2321ce755437f148dce0551 Taliri yaanzisha vituo 30 ufugaji

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASASI ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) imeanzisha vituo 30 wilayani Kongwa mkoani Dodoma kufanya utafiti wa kuzalisha malisho bora na kuwagawia wafugaji ili wazalishe mifugo bora itakayotoa maziwa, nyama na ngozi bora itakayouzika kimataifa.

Akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Profesa Olesante ole Gabriel aliyewatembelea ili kuona shughuli zao, Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI, Dk Eliby Shirima alisema lengo la kuanzisha vituo hivyo ni kuwa karibu na wafugaji kwa kutoa elimu ya kuzalisha malisho bora kuboresha ufugaji yao.

Alisema taasisi hiyo iliyoanza shughuli zake Kongwa mwaka 1947 inamiliki eneo la ekari 2,400 ambalo inalitumiwa kama shamba darasa la kuzalisha malisho bora na kutoa mafunzo kwa wafugaji ili wajifunze namna ya kulisha mifugo kwa kutumia malisho bora zaidi.

“Taliri yenye watumishi 27 na uhaba wa watumishi 34, inafuga ng’ombe 200 na mbuzi 303, imejenga mabanda ya namna ya kufuga na hivyo kusaidia jamii kujua namna bora ya ufugaji na ulishaji wa malisho bora,”alisema.

Alisema taasisi hiyo inafanya utafiti katika vijiji sita vya wilaya hiyo, kutoa elimu kwa wafugaji wenye mashamba wanane namna bora kuotesha malisho bora ili kupata mazao bora ya mifugo. Dk Shirima alisema pia taasisi hiyo imepeleka madume bora ya mbuzi yaliyonenepeshwa katika vijiji vya wafugaji wanaofuga kuwapatia mbegu bora ya mbuzi na madume hao yakirutubisha yanapelekwa makundi mengine.

Mfugaji wa ng’ombe za kienyeji, Mionaki Msingilili aliyepewa malisho ya ng’ombe aina ya Cenchius Ciliaris na Taliri alisema kabla ya malisho hayo na kuyapanda miaka miwili iliyopita alipata maziwa lita moja au mbili tu.

Baada ya kuanza kulisha mifugo yake majani hayo, sasa anapata maziwa lita sita hadi saba, kitendo ambacho kimeshangaza wanakijiji wa Msunjilile kata ya Sejeli walioshuhudia mageuzi ya ufugaji na wanaishukuru Taliri kwa elimu.

Akitoa ushauri kwa Taliri ambayo alifurahishwa na utendaji wake, Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, (Mifugo) Profesa Gabriel alisema wanatakiwa kushirikiana na NARCO kusambaza majani kwa wafugaji wabadilike na kufuga kisasa kwa kulisha malisho yenye lishe.

Alisema NARCO wenye ekari zaidi ya 600,001 nchini, wanaweza kuzitumia kupanda majani na kuwagawia wafugaji ili wapande kunenepesha mifugo yao itakayouzwa kwa bei kubwa sokoni.

Chanzo: habarileo.co.tz