Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takwimu zaonesha wafugaji wadogo ni wengi zaidi nchini

Ruyangwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Richard Ruyango

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takwimu zaonesha wafugaji wadogo ni wengi zaidi nchini Takwimu za sensa ya mifugo na uvuvi mwaka 2019-2020 zinaonyesha kuwa uzalishaji wa maziwa ya ng'ombe nchini Tanzania ni lita bil 3.13 kwa mwaka, kati ya hizo lita bil 3.11 sawa na 96.4% zinazalishwa na wafugaji wadogo ,ambapo lita bil 17.8 sawa na 0.6%hutoka mashamba makubwa , hivyo kwa mujibu wa takwimu hizo zinadhihirisha kuwa wafugaji wadogo ni wengi kuliko wakubwa na ndio wanaozalisha malighafi kwa wingi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Eng.Richard Ruyango katika Mafunzo ya siku mbili yanayoendelea Mkoani Arusha mafunzo ambayo yalioandaliwa na TBS, kwa wazalishaji,wasindikaji na wasambazaji wa maziwa, bidhaa zitokanazo na maziwa, na kuwataka kuzingatia kanuni Bora za matakwa ya viwango.

Aidha Ruyango ametoa rai kwa wajasiriamali hao, kutambua kuwa uzalishaji wa maziwa unahitajika kuwa bora,sambamba na kutambulika ubora wake kabla ya kupelekwa kwenye matumizi ya kinadamu, kwani itawasaidia kwa pamoja kuelewa uzalishaji unaokidhi viwango,ubora,na usalama ili kulinda Afya ya mlaji pamoja na kukuza uchumi wa taifa haswa katika suala la ushindani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live