Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takwimu sahihi kukuza uchumi wa wa viwanda

Uchumi Kupanda Takwimu sahihi kukuza uchumi wa wa viwanda

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashata Dkt. Hashil Abdallah amewataka wamiliki wa viwanda nchini kutoa ushirikiano katika kufanikisha utafiti wa shughuli za kiuchumi na kijamii wa mwaka 2023, ili kujenga uchumi shindani wa viwanda nchini.

Dkt. Hashil ametoa rai hiyo mkoani Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wasimamizi na wadadisi wa utafiti wa shughuli za kiuchumi na kijamii wa mwaka 2023 kwa Tanzania Bara.

Amewataka washiriki 527 wa mafunzo hayo kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi na mbinu za kitafiti ili kukusanya takwimu sahihi na zenye ubora na kuhakikisha wanakusanya taarifa zinazokidhi malengo yaliyokusudiwa ili kuiwezesha Serikali kutunga sera, kupanga mipango na kufuatilia utekelezaji wa programu mbalimbali za maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live