Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru kuchunguza vyama visivyolipa wakulima

Kilimo House Takukuru kuchunguza vyama visivyolipa wakulima

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Chrisitina Mndeme ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani humo kuchunguza vyama vya msingi 12 ambavyo vimeshindwa kuwalipa wakulima zaidi ya 900 kiasi cha Sh bilioni 2.5.

Pia ametoa wiki moja kuhakikisha makampuni mawili ya Mkwawa na Voedsel ambayo yalifunga mkataba na wakulima kwenye ununuaji wa zao la tumbaku ambapo wamepitiliza miezi minne bila kuwalipa wakulima.

RC Mndeme amesema hayo jana wilayani Kahama alipokuwa akiongea na viongozi wa chama kikuu cha ushirika wilayani humo (Kacu) na baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi.

"Vyama hivyo ni Kangeme, Kasela, Mbuni, Twiga Mapamba, Mihama Kabanga Mtakuja Iringabalimi, Nyakashatara, Kimumwe vimeshindwa kurejesha fedha kwenye mabenki kwa asilimia 100 waliyokopa nakushindwa kuwalipa wakulima”alisema Mndeme.

Mndeme alisema ilifanyika biashara huria isiyokuwa na uangalizi mzuri na imeonekana kuwatesa wakulima na kutopata haki hivyo mkuu wa wilaya alisimamie hili na waliohusika kusababisha hasara kwenye benki na wakulima wahojiwe. “Atakaye bainika kusababisha hasara hiyo achukuliwe hatua ya kufikishwa mahakamani na hakuna chama kitakachoanzishwa kipya bali vyama hivyo vifufuliwe upya hatuwezi kukubali Sh biloni 2.5 zipotee bure,”alisema Mndeme. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live