Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tafiti kung'arisha sekta ya madini

Vibali Madini (600 X 303) Tafiti kung'arisha sekta ya madini

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amesema serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) inafanya shughuli zake kwa ufasaha ili kuongeza tija katika Sekta ya Uvuvi nchini.

Dkt. Biteko amebainisha hayo jijini Dar es Salaam leo Oktoba 26, 2023, wakati wa maadhimisho ya Miaka 40 ya taasisi hiyo, ambapo ameitaka TAFIRI kuweka mkazo zaidi katika utafiti wa uvuvi kwenye Ukanda wa Bahari ya Hindi kwa kuwa bado mchango wake ni mdogo tofauti na mchango wa sekta hiyo kwenye upande wa maziwa.

Ametaka Sekta ya Uvuvi kuwa nyenzo ya kuondoa umasikini na kuvutia uwekezaji pamoja na kuchangia uwepo wa mazao ya uvuvi nje ya nchi.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema wizara imeweka mkakati kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 Sekta ya Uvuvi ichangie kwenye pato la taifa katribani kwa asilimia kumi tofauti na sasa ambapo inachangia kwa asilimia 1.7 pekee.

Ameongeza kuwa wizara inalenga kuweka mazingira mazuri na kuratibu ufugaji samaki kwa wingi ili kuzalisha zaidi kutoka tani laki tano kwa sasa hadi tani laki sita ifikapo mwaka 2025/2026.

Amesema ufugaji wa samaki ni kipaumbele kwa wizara na kwamba TAFIRI imesaidia kuondoa baadhi ya vikwazo vya ufugaji wa kwenye vizimba katika Ziwa Victoria kwa kufanya tafiti ya maeneo ya ziwa hilo ambayo yanafaa kwa ufugaji.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TAFIRI, Yahya Mgawe, ameiomba serikali kupitia kwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko kununua meli ya utafiti yenye thamani ya Shilingi Bilioni 6 ili kusaidia kurahisisha shughuli za utafiti katika Ukanda wa Bahari ya Hindi.

Amesema meli hiyo itasaidia pia kukuza Uchumi wa Buluu kwa kuainisha masuala mbalimbali yatakayochochea Sekta ya Uvuvi kukua zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live