Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taboa kuja na mfumo kununua tiketi kielektroniki

Taboa kuja na mfumo kununua tiketi kielektroniki

Tue, 11 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kutokana na kasi ya huduma kwa mifumo ya teknolojia, Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) kimetangaza zabuni ya utengezaji wa tiketi za kielektroniki zinazowezesha msafiri kuuliza ratiba ya safari, kulipia au kuweka ombi la kulipia tiketi kwa njia ya mtandao.

Kwa mujibu wa Taboa, mfumo huo utasaidia kupunguza matukio ya utapeli kwa wasafiri, kuboresha huduma za mabasi na bei halisi za safari kila njia ya safari za mikoani kupitia simu ya mkononi.

“Siku 14 baada ya tangazo tutakuwa na mkutano na TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) kujadili namna mfumo huo utakavyofanya kazi kwa ukaribu na mamlaka hiyo,” amesema Katibu Mkuu wa chama hicho, Enea Mrutu.

 

Amesema  mfumo huo utaanza siku chache zijazo na kwamba taasisi yoyote ya Serikali au mamlaka italazimika kupata taarifa za Taboa kupitia TRA.

 

Pia Soma

Advertisement
Amebainisha kuwa walikuwa wakitafuta mzabuni wa ndani kwa ajili ya kuchochea ajira katika sekta hiyo.

 

“Mfumo utaruhusu mwendeshaji kuratibu shughuli za ukatishaji wa tiketi zake. Tutaanza kama mfano  na kama mfumo ukifanikiwa tutautekeleza kwa nchi nzima,” amesema.

 

Mwishoni mwa mwaka 2019, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe alisema mfumo huo utakuwa ni njia pekee ya kuwezesha serikali kudhibiti ubora wa huduma na kuondoa malalamiko ya wamiliki na madereva wa mabasi katika biashara hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz