Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taasisi zapewa siku 41 kutoa gawio

88210 Fedha+pic Taasisi zapewa siku 41 kutoa gawio

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango nchini Tanzania, Dk Philip Mpango ametoa siku 41 kwa kampuni na mashirika kuwasilisha gawio au michango serikalini la sivyo bodi zake zitavunjwa.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa Novemba 24, 2019 mjini Dodoma  wakati akipokea gawio na michango kutoka kampuni na mashirika 79.

Dk Mpango ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Desemba 12, 2019 wakati akipokea gawio kutoka kwa kampuni na mashirika 13 yaliyotoa Sh4.285 bilioni.

“Wote ambao hawajaleta gawio ama mchango kwenye mfuko mkuu, kampuni, taasisi na mashirika yote ya umma ambayo Serikali imewekeza ikifika Januari 23 mwaka 2020 saa 6 usiku kama hawajaleta gawio wala michango ya kuingia kwenye mfuko mkuu bodi zake zitavunjwa,” amesema.

Amesema watatoa fursa nyingine kwa kampuni, mashirika na taasisi kupeleka gawio na michango yao kabla ya muda alioutoa haujaisha.

Chanzo: mwananchi.co.tz