Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taasisi za umma zatakiwa kujiunga na mfumo wa GePG

Wed, 12 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Wizara ya Fedha na Mipango imetoa miezi sita kwa taasisi zote za umma zisizotumia mfumo wa kielektroniki wa kukusanya mapato (GePG) kuanza kutumia mfumo huo.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba12, 2018 na kubainisha kuwa baada ya muda huo kupita utafanyika ukaguzi na kuwawajibisha maofisa masuhuli  wazembe kazini.

Akifungua  mkutano wa mwaka wa kwanza wa watumiaji wa mfumo huo naibu katibu mkuu wa wizara hiyo, Dk Khatibu Kazungu amesema kuwa ukaguzi huo utaanza kufanyika baada ya Juni, 2018.

Amesema watafanya ukaguzi wa ofisi zote za umma ili kubaini fedha zisizokusanywa na zisizopita kwenye mfumo wa GePG na kwamba ofisi itakayobainika kutotumia mfumo huo,  maafisa masuhuli watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

“Mnifikishie ujumbe wa kuzikumbusha taasisi ambazo bado hazijajiunga na GePG kuwa mpaka Juni 30, 2019 hakutokuwa na fedha yoyote ya umma itakayokusanywa nje ya mfumo huo. Wakati wa kujiunga na mfumo huo ni sasa,” amesema.



Chanzo: mwananchi.co.tz