Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Omar amezitaka taasisi zinazosimamia zao la Chai kushirikiana na wadau wote wa Chai kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza uzalishaji,tija na ubora wa zao hilo.
Agizo hilo amelitoa leo Novemba 13, 2023 wakati wa uzinduzi mnada wa Chai kwa njia ya mtandao uliofanyika jijini Dar es salaam na kuudhuriwa na wanunuzi,wauzaji wazalishaji na wakulima.
Amesema ili kuweza kufanikiwa lazima kuwekeza kwenye ubora na tija lakini pia wasindikaji wote wanapaswa kushiriki kwenye mnada wa Chai unaofanyika nchini.
“Wasindikaji wanapaswa kushiriki kuinua mnada wa Chai kwa kuunza angalau asilimia 15 ya Chai wanayozalisha na kuwakilisha mauzo ya moja kwa moja kwenye mnada huu”amesema Omar
Aidha amewataka pia kuchochea ushirikiano na nchi jirani zinazozalisha zao la Chai ili kuhamasisha kutumia mnada wa zao la Chai hapa nchini.
Ameongeza kuwa wadau wa zao la Chai wanapaswa kuhamasisha uwekezaji wa mnyororo wa thamani wa zao hilo pamoja na kuanzisha masamba mapya Chai na kujenga viwanda.
“Tukiweza kuoboresha Chai yetu vizuri na kuofanya kuwa Bora tunaweza kushawishi watu wengi na kuvutia uwekezaji.
Sambamba na hayo Dkt Omar amewataka wamiliki wa viwanda kuwalipa wakulima wadogo ili kuongezea hamasa kuendelea na kilimo cha zao hilo.
“Nielekeze wamiliki wote wa mashamba ambayo wameyatelekeza wahakikishe wanayafufua na kuyatunza vizuri na wahakikishe wanalima kwa tija na ubora unaotakiwa sokoni.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Chai Nchini, Mary Kipeja amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ufinyu wa bajeti kutangaza mnada kwenye masoko mpaya nje ya nchi.
Amesema kuanzishwa kwa mnada huo kutakuwa na manufaa makubwa kwa wakulima, wazalishaji na serikali kuongeza pato la Taifa kwa kutumia bandari ya Dar es Salaam na Tanga watengeneze ajira kwa vijana na wanawake.
“Taarifa za mauzo ya chai rakodi ya mwezi Julai hadi Oktoba ni tani 2584 asilimia 18 ilibaki nchini asilimia 82 ilipelekwa Mombasa nchini Kenya hivyo mnada kufanyaki nchini kutapunguza gharama kwa asilimia 50 na mkulima atapata faida,”amesema Kipeja.
Amesema bei elekeze kwaajili ya majani mabichi wakulima wadogo watanufaika na kupitia zao la chai watapata fedha na kufufua mashamba.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wazalishaji wa Chai Nchini (TAT), George Mwakamula amesema mnada huo utakuwa na mkubwa kwa wakulima wa chai na kwa manufaa ya Taifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Wadogo wa Chai, Felix Chole amesema kufanya mnada kwenye nchi nyingine wakati chai wanazalisha wenyewe mnada huo watanufaika wakulima.