Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taasisi za kilimo Tanzania mbioni kubadili mitalaa

86104 Pic+kilimo Taasisi za kilimo Tanzania mbioni kubadili mitalaa

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema inazungumza na taasisi za kilimo kubadili mitalaa li wanafunzi wa mwaka wa mwisho kabla ya kuhitimu kwenda vijijini wafanye mafunzo ya vitendo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Novemba 27, 2019 na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga katika kongamano la kilimo hai mjini Dodoma lililowakutanisha wabunge, wakuu wa wilaya na taasisi mbalimbali.

"Tunataka kuzungumza na taasisi zote zinazotoa mafunzo ya kilimo nchini tubadilishe mitalaa kuwawezesha wanafunzi wa mwaka wa mwisho kabla ya kuhitimu waende vijijini kufanya mafunzo.”

"Ili upate cheti tunataka uwe umesimamia zao fulani umelileta na unakuja kueleza umefanya nini na tumeona mafanikio yako, hapo sasa utastahili kutunukiwa kwamba wewe ni mtaalam wa mazao fulani," amesema Hasunga.

Amebainisha kuwa kufanya hivyo nchi itaondokana na upungufu wa maofisa ugani.

“Sio kwamba hatuna maofisa ugani wapo lakini wameishia mitaani. Hata wale wa zamani mabadiliko ni mengi na mahitaji ni mengi pia, hivyo tunahitaji wataalam wa kutosha na wenye ujuzi,” amesema Hasunga.

Chanzo: mwananchi.co.tz