Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taasisi za fedha zabanwa mikopo ya wakulima

WAKULIMA Taasisi za fedha zabanwa mikopo ya wakulima

Sat, 19 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imezitaka taasisi za fedha nchini kuweka masharti nafuu ya mikopo kwa wakulima ili waweze kukopesheka.

Akizungumza leo Februari 18, 2022 mkoani Katavi, Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema mikopo ya masharti nafuu itawasaidia wakulima kulima kwa tija na kuongeza uzalishaji wa mazao nchini.

“Ni wazi masharti ya mikopo inayotolewa na taasisi nyingi za fedha si rafiki kwa mkulima mdogo kukopesheka.” amesema Mavunde na kuongeza

“Ninafahamu kwamba taasisi za fedha zinaongozwa na sheria ya Benki Kuu juu ya masharti ya mikopo lakini ziangalie namna nzuri ya kuweka masharti nafuu kwa wakulima kukopesheka kirahisi pasipo kuathiri takwa la Benki Kuu.

“Mh Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo kwa taasisi za fedha kupunguza riba zao kwa mikopo ya kilimo na kwasasa tumeanza kushuhudia benki nyingi zikitoza riba isiyozidi asilimia 10 kwenye mikopo ya Kilimo….: “ Hi hatua kubwa katika kuelekea kuwa riba ya tarakimu moja kwenye mikopo ya Kilimo hapa nchini ili kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo” amesema Mavunde ambaye yupo mkoani katika katika ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa chini ya ufadhili wa Shirika la Mapinduzi ya Kijani Barani Afrika (AGRA).

Awali wakizungumza kwa nyakati tofauti mkulima Aniceth Gosberth na muuzaji wa pembejeo za kilimo Eutropia Sangu wameiomba serikali isaidie ulegezaji wa masharti ya mikopo kwa taasisi za fedha ili wakopesheke kwa kuwa wanaamini wakipata mitaji zaidi wataweza kuimarisha kilimo na kuongeza tija.

Ziara hiyo inayoongozwa na Mjumbe wa Bodi ya AGRA na Rais Mstaafu Dr.Jakaya Kikwete pamoja na Makamu wa Rais wa AGRA Aggy Konde imehitimishwa leo baada ya kukagua miradi zaidi ya 20 katika mikoa ya Iringa,Mbeya Songwe, Rukwa na Katavi ambapo zaidi ya wakulima,wauza pembejeo na wasindikaji 100,000 wamenufaika na ufadhili wa AGRA kupitia huduma mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live