Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taasisi za fedha ni muhimili wa kukuza kampuni za kati

24075 100+PIC TanzaniaWeb

Sat, 27 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi mkuu wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker amesema ni muhimu kwa kampuni za kati kushirikiana na taasisi za fedha nchini ili zikue vizuri.

Bussemaker amesema hayo leo, Oktoba 25 katika hafla ya kuzitambua kampuni 100 bora za kati (Top 100) kwa mwaka 2018.

"Kampuni za kati ndiyo uti wa mgogo wa uchumi wa nchi ndiyo maana tupo hapa kusherekea mafanikio yenu. Tuna imani mtakuwa kampuni kubwa baada ya muda, kufika huko ni muhimu kushirikiana na benki ndiyo maana nipo hapa," amesema Bussemaker.

Amesema NMB inatarajia kuona kampuni za kati zilizopo na zitakazoanzishwa zinakuwa wateja wa benki hiyo.

Aidha amezitaka kampuni kuchangamkia matumizi ya teknolojia kwani ndio siri ya mafanikio katika zama hizi.

Mgeni rasmi katika mashindano hayo yanayofanyika kwa awamu ya nane sasa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema asilimia 90 ya uchumi wa Tanzania kwa sasa unategemea viwanda vya kati.

Chanzo: mwananchi.co.tz