Menu ›
Biashara
Tue, 10 Aug 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mfumko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai 2021 umeongezeka hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2021.
Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Makazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja amesema leo Jumatatu Agosti 9, 2021 wakati akitoa taarifa ya faharisi za bei za Taifa kwa Julai 2021.
Amesema hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2021.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live