Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TVET kutoa fursa za ajira

Katambiz TVET kutoa fursa za ajira

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi amewataka washiriki wa maonesho ya Pili ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) kutumia maonesho hayo kama sehemu ya kujikuza kiuchumi.

Akizungumza jijini Arusha yalipokuwa yakifanyika maonesho hayo Katambi amesema, mafunzo ya ufundi stadi yanawasaidia vijana kupata ujuzi wa kazi mbalimbali za kiufundi na kukuza ajira.

Amewataka washiriki wa maonesho hayo ya TVET kutumia vema fursa zilizotokana na kukutana, kubadilishana mawazo, ujuzi na maarifa katika kutimiza ndoto zao.

Aidha, Naibu Waziri Katambi ameongeza kuwa stadi za kukuza ujuzi ni nguzo bora kwenye elimu katika vyuo mbalimbali.

"Changamoto ya ajira tunaweza kuitatua tu pale ambapo tutakuwa na mipango madhubuti na mikakati endelevu ya kuwasaidia vijana wanapofika vyuoni wapewe stadi zinazowasaidia kukuza ujuzi,” amesema Naibu Waziri Katambi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live