Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TULONGE KILIMO : Huu hapa umuhimu wa mashamba darasa

47004 Pic+shamba

Mon, 18 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pamoja na mwamko walionao Watanzania kulima na kufuga, wengi wao wanakosa maarifa sahihi ya kusimamia miradi yao.

Kimsingi, unapokosa maarifa sahihi ya kilimo au ufugaji, mradi utakaoufanya lazima uwe wa kiholela na hivyo mwishowe kutokuwa na tija iliyokusudiwa.

Kwa kuwa wakulima na wafugaji wengi hawana muda wa kwenda darasani, hasa kwa kuzingatia pia hakuna ulazima wa kufanya hivyo, bado iko haja ya kuwa na mashamba darasa katika maeneo mbalimbali ili yawe chachu ya Watanzania kujifunza.

Mdau wa kilimo, Rajabu Kalungwana anasema, Shamba darasa ni kutumia ardhi kwa ajili ya kufundishia wakulima kwa vitendo ili kuonyeshea teknolojia  mpya au aina mpya ya mbegu na jinsi ya kuzitumia.

Anasema kisheria shamba darasa linatakiwa kuwa na ukubwa kuanzia ekari moja na kuendelea, japo  pia halitakiwi kuwa kubwa zaidi.

Umuhimu wa shamba darasa

Shamba darasa linasaidia wakulima kufahamu teknolojia mpya za kilimo kama vile mfumo wa  umwagiliaji wa matone,ulimaji wa mazao bila kutumia udongo na nyinginezo.

Kupitia shamba darsa mkulima anajifunza aina mpya za mbegu za mazao na jinsi ya ulimaji wake pamoja na utunzaji.

Kwa mfano mtu anayetaka kulima matikiti kwa kutumia shamba darasa anaweza kushauriwa aina bora ya mbegu na mifumo mbalimbali ya upandaji, umwagiliaji, uwekaji dawa na usimamizi wa mazao yake.

Rashidi Hassani anayelima matunda mkoani Tanga anasema ipo haja ya kutoa elimu kwa wakulima kupitia mashamba darasa, kwa sababu wakulima wengi wanashindwa kufikia malengo yao kwa kukosa elimu sahihi ya kilimo.

Anasema shamba darasa ni zaidi ya darasa la kawaida,  kwani linafungua nafasi kwa mtu ambaye hajui mambo ya msingi kuhusu kilimo.

Lakini pia shamba darasa ni  jukwaa la kuwakutanisha wakulima na wataalamu,  kufahamiana na kubadilishana uzoefu kuhusiana na kilimo.



Chanzo: mwananchi.co.tz