Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TTCL, TOSCI yawatangazia neema wakulima Tanzania

68929 Pic+ttcl

Tue, 30 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesaini mkataba wa makubaliano na Taasisi ya Udhibiti wa ubora wa Mbegu (TOSCI) ili kuweza kuwawezesha wananchi kufanya uhakiki wa pembejeo kwa kutumia TTCL Hakiki kabla ya kupanda.

Mkataba huo wa makubaliano wa mwaka mmoja umesainiwa leo Jumanne Julai 30, 2019.

Akizungumza katika hafla ya hiyo, Mkurugenzi mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema itaweka urahisi kwa wananchi kuwa na uhakika wa kile wanachopanda tofauti na zamani.

“Kukiwa hakuna ubora wa mbegu huko ndiyo tunaanza kupoteza tija ya kilimo kwa sababu sekta hii inaajiri zaidi ya asilimia 70 ya wananchi sasa kusainiwa kwa mkataba huu kutaweka uhakika wa ubora wa mbegu wanayokwenda kutumia kwa ajili ya uzalishaji wa mazao yao ili waweze kuendana na ajenga ya Tanzania ya viwanda ifikapo 2025,” amesema Kindamba

Akielezea jinsi itakavyokuwa inafanya kazi, Kindamba amesema mkulima ataweza kutuma namba zilizopo katika nembo Tosci katika mbegu na kuzituma kwa ujumbe mfupi wa maandishi za kawaida na kupewa majibu au kutumia QR code kwa watumiaji wa simu janja (smartphone) ili kupata majibu.

Naye Mkurugenzi mkuu wa Tosci, Patrick Ngwediagi amesema licha ya kuwa walijitahidi kufanya ukaguzi kila mara ili kuhakikisha wanaondoa mbegu bandia lakini bado kulikuwa na watu wanaofanya udukuzi.

Pia Soma

“Hata kama aliye athirika ni mmoja lakini nyuma yake kuna wengi waliokuwa wanategemea anachokizalisha, logo tulizokuwa tunaweka kuna watu walikuwa wanazidukua na kutengeneza kama zile na ilikuwa ngumu kutambua.” Amesema Ngwediagi

Chanzo: mwananchi.co.tz