Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TTB yaonya athari za mifuko ya plastiki ufukweni

11240 Pic+utalii TanzaniaWeb

Fri, 10 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Watanzania wametakiwa kuacha kutupa taka hasa za plastiki kwenye maeneo wanayoishi kwa kuwa baadaye taka hizo husafirishwa na maji mpaka kwenye vyanzo vya maji na fukwe.

Wito huo umetolewa leo Ijumaa Agosti 10, 2018 na Bodi ya Utalii nchini (TTB) ambayo imeanzisha kampeni ya kufanya usafi katika maeneo ya fukwe kwa ajili ya kuvutia utalii wa fukwe kwa wazawa na wageni.

Mkuu wa kitengo cha idara ya udhibiti wa leseni wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Rosada Msoma ambaye ameshiriki kusafisha ufukwe wa Ramada Resort, amesema ana imani kampeni hiyo itakuwa endelevu kwani ni miongoni mwa mipango ya Serikali kuvutia utalii wa fukwe.

“Fukwe zikiwa safi zitavutia utalii mbalimbali wanaopenda matembezi lakini pia kwa wazawa ni fursa ya kufanya biashara,” amesema Msoma.

Mkurugenzi wa masoko wa TTB, Ernest Mwamaja amesema fukwe nyingi hazipo katika hali ya usafi na uchafu wake kwa asilimia kubwa ni makopo ya plastiki yanayoletwa na maji yanayotiririka.

“Kuna haja ya kuongeza uelewa miongoni mwa watu ikiwa ni pamoja na kuwaasa kuacha kutupa taka za plastiki hovyo , madhara yake ni makubwa na lengo letu ni kuongeza utalii kufikia idadi ya watalii milioni mbili kwa mwaka ifikapo 2020,” amesema Mwamaja.

Kwa upande wake mkurugenzi wa masoko wa Ramada Resort, Bharath Swarup amesema ni jambo jema kuona TTB inawashirikisha wadau katika kampeni kama hiyo ambayo inalenga kutunza mazingira ya fukwe.

“Kupitia fukwe ambazo zimetunzwa vizuri Serikali inaweza kupata mapato ya kodi lakini kama fukwe zimechakaa haziwezi hata kuvutia wageni/watalii,” amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz