Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TSN yajivunia ushiriki maonesho ya madini

6fbd3734bcbe7f2fd12d8c05f3bf8c2f TSN yajivunia ushiriki maonesho ya madini

Fri, 25 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya HabariLEO, Daily News, SpotiLeo na DaliyNews Digital, inajivunia kuwa wadau muhimu wa maonesho ya tatu ya kimataifa ya teknolojia na uwekezaji kwenye sekta ya madini mkoani Geita.

Ofisa Mauzo na Masoko wa TSN, Goodluck Chuwa, alimweleza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telak alipotembelea banda la TSN jana kuwa Kampuni ya Magazeti ya Serikali ni wadau muhimu kwa maendeleo ya Mkoa wa Geita.

Chuwa alisema kuwa TSN ilifanya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkaoni Geita mwaka 2018 ambalo limekuwa chachu kwa uongozi wa Mkoa wa Geita kuratibu maonesho ya madini kwa mafanikio.

“Hata soko kuu la dhahabu la Mkoa wa Geita ni matokeo ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji ambalo TSN ililifanya katika mkoa huu wa Geita mwaka 2018, tunajivunia kuwa wadau wa maendeleo makubwa yanayopatikana mkoani hapa," Chuwa alimweleza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Chanzo: habarileo.co.tz