Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TSB yapiga marufuku Amcos kuchangisha mbegu za mkonge

194e58ded0e8c62f46d6621fb939eb5f TSB yapiga marufuku Amcos kuchangisha mbegu za mkonge

Sun, 24 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), imevipiga marufuku vyama vya ushirika vya zao la mkonge, Amcos kuchangisha wakulima fedha kwa ajili ya usambazaji wa mbegu kwa wakulima wadogo wa zao hilo.

Aidha, Bodi hiyo ilisema mbegu hizo zitawafikia wakulima katika maeneo yao bila ya gharama zozote lengo ikiwa ni kuongeza hamasa kwa wakulima kulima zao hilo kwa wingi na kwa ufanisi zaidi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge, Saddy Kambona alitoa kauli hiyo jana baada ya kikao na ukaguzi wa Shamba la Kibaranga lililopo wilayani Muheza mkoani Tanga.

Kambona alisema serikali imeipatia Bodi ya Mkonge fedha kwa ajili ya mbegu na zitasambazwa kwa wakazi wote wa Kibaranga na kwa maelekezo ya serikali mbegu zitamfikia mwananchi kwenye kijiji chake bila kuchangia gharama yoyote.

"Asichangishwe fedha mwananchi yeyote ili kupata mbegu labda kama mnafanya masuala mengine ya ulinzi wa mbegu na vitu kama hivyo, lakini si gharama za kufikishiwa mbegu Kijiji cha Darajani au kijiji chochote kingine,” alisema.

Awali mwenyeki wa Kijiji cha Darajani, Makende Maziku alisema wakulima wa mkonge katika kijiji hicho wamepokea ofa ya mbegu za mkonge vizuri na kusisitiza kasi zaidi ya upatikanaji wa mbegu hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Amcos ya Kibaranga, Paulo Haule alisema utaratibu uliokuwapo ni kuwa mbegu zinaishia Makao Makuu ya Amcos.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live