Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRC yataka nauli za treni zipande, wadau wapinga

TRC Nauliiii Nauliii TRC yataka nauli za treni zipande, wadau wapinga

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Ardhini (Latra CCC) wameshauri viwango vya nauli katika usafiri wa reli zibaki kama zilivyo hadi hapo watakapo boresha huduma zao.

Mapendekezo hayo yametolewa baada ya watuamiaji wa usafiri huo kueleza changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ugumu wa upatikanaji wa tiketi.

Akizungumza katika mkutano wa wadau uliofanyika kwa ajili ya kupendekeza viwango vipya vya nauli leo Ijumaa, Agosti 19, 2022, Kaimu Mtendaji wa Baraza la latra CCC, Leo Ngowi amesema baada ya kuchambua maoni na kufanya utafiti waliweza kubaini huduma zinazotolewa TRC bado ni ndogo hivyo wanatakiwa kuongeza uzalishaji wa huduma zao maana uhitaji bado ni mkubwa.

"Hakuna haja ya kuomba ongezeko la nauli kwa sababu wanafursa ya kuongeza uzalishaji," amesema Ngowi

Hata hivyo, amesema TRC wanatakiwa waboreshe huduma zao kwa kuondoa kipindi kirefu cha abiria kusubiri kituoni.

"Waruhusu abiria kukata tiketi kwa njia ya mtandao kwa kuwa itarahisiha mambo," amesema.

Pia, amesema wanakubali mafuta yamepanda bei lakini kwa upande wa utendaji wa TRC bado ni hafifu, endapo watafanya mambo yao kwa ufasaha pamoja na kuboresha huduma zao watakubali kukaa mezani kujadiliana.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), Hassan Mchanjama amesema TRC hawana sababu ya kupandisha nauli kwa asilimia 15, maana bado kunachanyamoto katika huduma zao.

"TRC wanatakiwa wajipange vizuri katika kudhibiti mapato, maana abiria wanajazana kwenye mabehewa ya treni," amesema Mchanjama.

Kwa upande wake, TRC kupitia Kaimu mkurugenzi wake, Hassan Shabani ambae amemwakilisha mkurugenzi wa maendeleo ya biashara amesema nia yao ni kupandisha nauli kwa asilimia 15 kwa sababu ya ongezeko la bei ya mafuta.

"Kwa safari zote za ndani kwa gharama za mafuta zimepanda karibu kwa asilimia 38 lakini nauli ya treni imekuwa ni ile ile," amesema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluhu amesema wao kama latra jukumu lao ni kupokea mapendekezo na kwenda kuyafanyia kazi, hivyo mapendekezo haya hayataishia Dar es Salaam kwani hata mikoa mingine kama Kigoma, Mwanza watapewa nafasi ya kutoa mapendekezo yao.

Akihitimisha mjadala huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija ambae ndie alikua mgeni rasmini amesema wadau wote waliojitokeza kwa ajili ya majadiliano wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha madai yao kwa ufasaha.

"Maoni yanayotolewa hapa yatakuwa ni shirikishi hivyo, tuhakikishe tunatoa maoni ambayo yamekidhi mahitaji ya wananchi wote," amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live