Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRC yaongeza safari mikoa ya Kaskazini

8c068eaf3bd185a97538f07e3a8041c7 TRC yaongeza safari mikoa ya Kaskazini

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeongeza safari ya treni kwenda mikoa ya Kaskazini ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha. Taarifa ya TRC kwa vyombo vya habari ilieleza jana kuwa mabadiliko hayo yalianza juzi kwa kuwa na safari tatu kwa wiki kutoka safari mbili za awali.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa kuanzia sasa treni hiyo itafanya safari zake katika siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa saa nane na nusu mchana kutoka Dar es Salaam kwenda Kaskazini.

TRC ilieleza kuwa treni kutoka Kaskazini kwenda Dar es Salaam itafanya safari zake siku za Jumanne, Alhamisi na Jumamosi ikitoka Arusha saa nane na nusu mchana.

Ilisema kuongezwa kwa safari hizo kumetokana na kuongezeka kwa idadi ya abiria hususani kipindi hiki ambapo bei za usafiri mwingine yakiwemo mabasi imepanda hivyo kuwafanya wasafiri kutafuta unafuu wa bei kufanikisha safari zao.

Aidha, Shirika hilo limewataka wananchi wanaokusudia kusafiri kwa kutumia treni hiyo kukata tiketi za safari katika stesheni zote za TRC au kwa njia ya mtandao wa shirika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live