Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRC wabanwa kasi usimamizi wa miradi

Pic Reli Data.jpeg TRC wapewa maagizo kuongeza kasi usimamizi wa miradi

Tue, 19 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile na Wakuu wa Wizara hiyo leo Septemba 18,2023 wametembelea Shirika la Reli Tanzania (TRC).

Pamoja na kujitambulisha pia ilikuwa fursa kufahamu kwa kina majukumu ya Shirika, kazi wanazofanya ikiwemo utekelezaji wa miradi ya Kimkakati na mipango ya shirika.

Akizungumza katika ziara hiyo, Kihenzile ameitaka TRC kuongeza kasi ya usimamizi wa miradi na kuzingatia thamani ya fedha.

" Maono ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ni kuona taifa letu linakuwa kitovu cha usafirishaji kwenye Ukanda wetu wa Afrika Mashariki, Kusini na Kati kwa kutumia fursa ya kimkakati tuliyopewa na Mungu." Amesema Kihenzile na kuongeza

"Hivyo ni lazima kuongeza kasi zaidi katika kuhudumia mizigo mingi na abiria wengi kutoka bandarini na kuleta mizigo bandarini." Amesema

Amesema, Wizara ya Uchukuzi chini ya Waziri wake Prof Makame Mbarawa wataendelea kuweka mkazo mkubwa kwenye kuboresha usafiri wa reli, viwanja vya ndege, Meli na kufanya mageuzi makubwa kwenye bandari ili kuongeza tija.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live