Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRC mbioni kuongeza safari treni ya abiria Dar-Moshi

88216 Treni+pic TRC mbioni kuongeza safari treni ya abiria Dar-Moshi

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema lipo mbioni kuongeza safari za treni ya abiria kati ya Dar es Salaam na Moshi kutoka mbili kwa wiki hadi tatu.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Desemba 12, 2019 na mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Masanja Kadogosa katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia utendaji wa shirika hilo tangu mwaka 2015.

Amesema Watanzania wamepokea kwa shauku treni hiyo, kwamba kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka wamepata maoni mengi kuhusu kuongezwa kwa safari hizo.

“Hii ni treni ya Watanzania wametoa maoni na tumeyapokea tumeyafanyia kazi, tutaona ni jinsi gani tunajipanga kuhakikisha inakwenda Moshi mara tatu kwa wiki na kurudi Dar mara tatu,”

Kadogosa pia amezungumzia ukarabati wa mabehewa ya shirika hilo na kueleza kuwa wana nia ya kuyafufua na kuyaweka katika hali nzuri ili yatumike.

Kwa sasa treni hiyo inatoka Dar es Salaam kila Ijumaa na Jumanne na Moshi kila Jumatano na Jumamosi.

Hata hivyo jana mkuu wa kitengo cha habari na uhusiano wa shirika hilo, Jamila Mbarouk alilieleza Mwananchi kuwa  wamelazimika kuongeza safari tatu kutoka mbili kutokana na wingi wa abiria.

“Kutokana na uhitaji wa abiria kuanzia Jumatatu tumeongeza safari, itakuwa inaondoka Dar es Salaam Jumatatu, Jumatano na Ijumaa na kuondoka Moshi kuja Dar es Salaam kila siku ya Jumanne, Alhamisi na Jumamosi.”

“Uhitaji wa abiria  umekuwa mkubwa tofauti na tulivyofikiria na kwa kuwa tumejipanga katika hili tulichofanya cha kwanza ni kuongeza siku za kusafiri. Wakizidi tutaongeza mabehewa kutoka yaliyopo sasa,” amesema Jamila.

Chanzo: mwananchi.co.tz