Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRC kununua behewa 1430 za mizigo

TRC  Mkataba (600 X 373) TRC kununua behewa 1430 za mizigo

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la reli Tanzania TRC limesaini mkataba wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 127.2 sawa na Tsh. bilioni 292.1 na Kampuni ya CRRC international ya nchini China kwa ajili ya ununuzi wa behewa 1430 za mizigo ya reli ya kisasa

Wakisaini mkataba huo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa amesema utengenezwaji wa behewa hizo utachukua muda wa miezi 12 hadi kukamilika kwake ambapo zitakuwa na mjumuiko wa kubeba bidhaa mbalimbali ikiwemo behewa za kubeba magari, mifugo, mafuta na bidhaa mchanganyiko

Kwa upande wake Waziri wa ujenzi na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa na Mkurugenzi wa bodi wa TRC wamesema serikali imedhamiria kuhakikisha sekta ya usafirishaji wa mizigo unaleta tija na kuongeza pato la Taifa.

Aidha Mbarawa amelitaka shirika hilo kuhakikisha linasimamia ubora wa behewa hizo na mradi ukamilike kwa wakati waliokubaliana kwenye mkataba.

Behewa hizo zinatarajiwa kukamilika na kuwasili nchini mapema Februari 25 mwaka 2023 ambapo zinatarajiwa kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kuongeza tija katika mzunguko wa biashara nchini.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 25 na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia.

Siku hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Lugano Kasebele ilidaiwa kuwa Januari 5, maofisa hao wa polisi walimuua Musa Hamis Hamis (25), mkazi wa Nachingwea mkoani Mtwara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live