Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRC: Sio kila sehemu itahitaji umeme

Sgr 1140x640 TRC: Sio kila sehemu itahitaji umeme

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Reli Tanzania(TRC) limewaondoa hofu wananchi kuhusu kukatika kwa umeme wakati wa safari za treni ya umeme likisisitiza kuwa limeweka mifumo mizuri kuwezesha safari hizo kufanyika na kwamba sio kila maeneo yanahitaji umeme.

Mkurugenzi wa Ishara, Mawasiliano na Umeme TRC, Mhandisi Mateshi Titto, amesema kuwa ujenzi wa reli hiyo pia ulizingatia hali ya upatikanaji wa umeme na kwamba kuna vichwa vitakuwa na uwezo wa kutumia diseal ili pale hitilafu za umeme zikitokea safari ziendelee.

Akizungumza wakati wa majaribio ya safari hizo, leo Februari 26, Titto amesema mradi huo mkubwa kuwa kufanyika nchini umeweka mfumo wa jenereta ambazo zitatumika katika vituo kusaidia upatikanaji wa umeme wakati wa hitilafu za umeme.

“Tunatumia umeme wa gridi ya taifa ambao vyazo vyake ni vingi. Ingawa tayari wameanza kuingiza umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, umeme uliokuwepo ulikuwa unatutosha kuendesha treni hii,” amesema Mhandisi Titto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live