Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRC: Kichwa kilikwamisha safari za SGR

Masanja Kadogosa, Kamati Kusafiri Na SGR TRC: Kichwa kilikwamisha safari za SGR

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema safari za reli katika reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro zimechelewa kuanza kwa sababu ya kuchelewa kupatikana kwa kichwa cha treni, ambacho kwa sasa kimepokelewa nchini.

Kadogosa amesema kufuatia kupokewa kwa kichwa hicho na mabehewa zaidi ya 40, majaribio ya reli hiyo yataanza muda wowote kutoka sasa, ambapo wakijiridhisha kuwa kichwa kinakidhi vigezo ikiwemo kwenda kasi ya kilomita 160 kwa saa, safari ambazo umma unazisubiri kwa hamu zitaanza.

Aidha, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuimarisha usafiri wa reli, akisema kwa muda wa miaka nane aliyohudumu kwenye sekta ya reli, kwa mara ya kwanza ameshuhudia kiongozi mkuu wa nchi anakwenda kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli ya Kusini.

Ameeleza hayo Ikulu, Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu mpango wa Tanzania kujenga reli ya ushoroba wa Kusini kutoka Bandari ya Mtwara hadi Mbamba Bay, ujenzi ambao unaendana na upanuzi wa bandari ya Mtwara, ujenzi wa kongani ya viwanda na kujenga kinu cha kuchenjulia madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live