Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yazindua kampeni risiti EFD

EFD EFD TRA yazindua kampeni risiti EFD

Sat, 16 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mwanza imezindua kampeni ya ‘Tuwajibike’ yenye lengo la kutoa elimu na kuwakumbusha wauzaji wa bidhaa na wanunuzi kutoa na kudai risiti halali za EFD mashine.

Kampeni hiyo imezinduliwa leo Ijumaa Septemba 15 katika ofisi za Mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kutambulisha kampeni hiyo kwa waandishi wa habari na baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo, Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza, Ernest Dundee amesema kampeni hiyo itakuwa endelevu.

Ameawma ina malengo makuu matatu ikiwemo kuwakumbusha na kuwahamasisha wanunuzi wa bidhaa na huduma mbalimbali kudai risiti halali za EFD pamoja na kuzikagua ili kubaini kama zina thamani halisi ya kiasi cha fedha kilicholipwa.

” katika kampeni yetu hii ya tuwajibike Watumishi wa Mamlaka ya Mapato watakuwa wanapita katika maeneo tofauti na kukagua na kuhakikisha Kila muuzaji au mnunuzi anatoa na kudai risiti na Kwa mnunuzi uhakikishe kabla hujatoka eneo ulilonunua bidhaa dai risiti Ili kuepukana na usumbufuutakaoweza kujitokeza” amesema Dundee

Amesema kampeni hiyo pia imelenga kufuatilia utoaji wa risiti halali za EFD katika maeneo mbalimbali ya biashara pamoja na kuchukua hatua kwa wauzaji wasiofuata sheria katika utoaji wa risiti hizo.

Hata hivyo kuwachukulia hatua za kisheria kwa wafanyabiashara wanaotumia risiti moja wakati wa kusafirisha mizigo pamoja na kuuza risiti pasipokuwa na manunuzi yoyote.

Ameeleza katika kampeni hiyo watumishi wa Mamlaka hiyo watapita katika maeneo mbalimbali ya biashara ili kukagua kama mnunuzi amepewa risiti halali.

Mfanyabiashara kutoka Mwanza, Upendo Mwakyolile ni wafanyabiashara kutoka amesema kuna faida kubwa kutoa risiti kwani wakati wa kupewa makadilio ya kodi inakuwa ni rahisi na mpangilio mzima wa mauzo unaonekana hata kama hujaweka kumbukumbu kwenye kitabu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live