Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TRA yawatoa hofu wachimbaji wadogo

Mud Matope Madini TRA yawatoa hofu wachimbaji wadogo

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA), imewatoa hofu wachimbaji wadogo mkoani Geita juu ya kodi ya asilimia mbili ya mauzo itakayoanza kutozwa kwani mabadiliko yamezingatia maoni ya kamati za wachimbaji. - Ofisa Kodi wa TRA Mkoa wa Geita, Sadick Rutenge ameeleza hayo wakati akizungumza na mashirikisho ya wachimbaji wadogo, wafanyabiashara na madalali wa madini katika semina maalum mjini Geita. - Rutenge amesema mabadiliko ya sheria yanayofanywa na serikali katika sekta ya madini yanalenga kuongeza tija kwa kupunguza utitiri wa tozo na kuwatia motisha wachimbaji kulipa kodi hivo wayapokee. - “Nia na makusudi ya sheria hii, tuliweza kugundua kwamba kuna wachimbaji wengi ambao wanafanya biashara ya madini ambao kimsingi inakuwa ni ngumu kutunza kumbukumbu zao za uchimbaji. - “Kwa hiyo sheria hii imekuja kwa lengo la kuweza kumfanya mchimbaji mdogo atakapokuwa ameuza madini yake aweze kulipia hiyo asilimia mbili,” amesema na kuongeza; - “Sheria hii inawahusu wachimbaji wote ambao wanazalisha dhahabu kwa kutumia leseni ya awali (Primary Mining Licence) pamoja na wale ambao hawana leseni za uchimbaji (artisanal mining). - “Tumewaambia kabisa kwamba katika leseni walizonazo wenyewe ndio watakuwa wanakata ile asilimia mbili pamoja na kuilipa kwa serikali kwa sababu wao ndio wanunuzi ambao serikali imewaamini.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live